Al-Anfaal 8:35
الأنفالوَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ ٱلْبَيْتِ إِلَّا مُكَآءً وَتَصْدِيَةً ۚ فَذُوقُوا۟ ٱلْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ
Na hakukuwa kuswalia kwao kwenye hiyo Nyumba (Al-Kaaba) isipokuwa ni kupiga miunzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mkikufuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga miunzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru. [35]
[35] Na maombi yao kwenye Nyumba hii Tukufu (Al Kaaba) si chochote ila ni kupiga myunzi na makofi. Ilivyo kuwa hiyo ndiyo hali yenu, basi wacha mauti yakupateni, na yaonjeni katika uwanja wa vita, upate kubaidika (kuwa mbali) ushirikina kutokana na Al Kaaba. Na kuuliwa huko kwenu ni kwa sababu ya ukafiri wenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakukuwa kuswali kwao kwenye Msikiti wa Harãm isipokuwa ni kupiga miluzi na kupiga makofi, basi onjeni adhabu ya kuuawa na kutekwa siku ya Badr kwa sababu ya kukanusha kwenu na vitendo vyenu ambavyo hakuna mwenye kujitokeza kuvitenda isipokuwa makafiri wenye kukataa upweke wa Mola wao na utume wa Nabii wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net