Al-Anfaal 8:36
الأنفالإِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ لِيَصُدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ ۗ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ
Hakika wale waliokufuru hutoa mali zao ili waizuilie Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa, kisha zitakuwa majuto juu yao, kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam. [36]
[36] Hakika hao wanao zipinga Ishara za Mwenyezi Mungu na wanamshirikisha na miungu mingine, hutoa mali yao ili wawazuie watu wasiifuate Imani ya Haki! Nao wataendelea kutoa hayo mali, kisha hayo mali, kwa kuwapotea bure bila ya pato walitakalo, yatawaletea majuto na machungu. Na katika uwanja wa mpambano watashindwa hapa duniani, na kisha watakusanywa wote katika Jahannam, wakibaki na ukafiri wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika ya wale wenye kukanusha upweke wa Allah Mtukufu na wakamuasi Mtume Wake wanatoa mali yao kuwapa washirikina na watu wa upotevu wanaofanana na wao ili kuzuia njia ya Allah Mtukufu isifuatwe na kuwazuia Waumini wasimuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake. Basi watatoa mali yao kwa lengo hilo, kisha mwisho wa utoaji wao utakuwa ni majuto na hasara juu yao, kwani mali yao yatamalizika na hawatapata wanaoyatarajia ya kuzima nuru ya Allah Mtukufu na kuzuia njia Yake isifuatwe, kisha mwishowe Waumini watawashinda. Na wale waliokufuru watakusanywa wapelekwe kwenye Jahanamu waadhibiwe humo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net