Al-Anfaal 8:37
الأنفاللِيَمِيزَ ٱللَّهُ ٱلْخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِ وَيَجْعَلَ ٱلْخَبِيثَ بَعْضَهُۥ عَلَىٰ بَعْضٍ فَيَرْكُمَهُۥ جَمِيعًا فَيَجْعَلَهُۥ فِى جَهَنَّمَ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ
Ili Mwenyezi Mungu awapambanue waovu kutokana na wazuri, na awaweke waovu juu ya waovu wengine, na awarundike wote pamoja, na awatie katika Jahannam. Hao ndio waliohasirika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili Mwenyezi Mungu apate kuwa pambanua walio waovu na walio wema, na kuwaweka waovu juu ya waovu wengine, na kuwarundika wote pamoja, na kuwatupa katika Jahannam. Hao ndio walio khasirika. [37]
[37] Kwa kushindwa makafiri duniani na kuadhibiwa Motoni Akhera Mwenyezi Mungu anapambanua aliye khabithi wa roho na vitendo na maneno, awe mbali na aliye mwema wa roho yake na moyo wake. Na awafanye wale waovu makhabithi wapandane wenyewe kwa wenyewe, huyu juu ya huyu, na awatie Motoni Siku ya Kiyama. Na hao washirikina mafisadi ndio wenye kukhasiri peke yao, duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Atawakusanya na Atawatweza hawa ambao walimkanusha Mola wao na wakatoa mali yao kuwazuia watu kumuamini Allah Mtukufu na kuzuia njia Yake isifuatwe, ili Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Apate kukipambanua kichafu na kizuri, na ili Ayakusanye Allah Mtukufu mali ya haramu, yaliyotumiwa kuwazuia watu na dini ya Allah Mtukufu, Ayaweke baadhi yake juu ya mengine yawe yamekusanyikana na kupandana kisha Ayatie kwenye Moto wa Jahanamu. Makafiri hawa ndio wenye kupata hasara duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net