Al-Anfaal 8:38
الأنفالقُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِن يَنتَهُوا۟ يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ وَإِن يَعُودُوا۟ فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ ٱلْأَوَّلِينَ
Waambie wale waliokufuru ikiwa watakoma, watasitiriwa yale yaliyokwisha pita. Na wakiyarudia, basi hakika imekwisha pita mifano ya wa mwanzo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waambie wale walio kufuru: Wakikoma watasamehewa yaliyo kwisha pita. Na wakiyarudia basi imekwisha pita mifano ya wa zamani. [38]
[38] Hakika juu ya vitisho hivi, mlango wa matarajio ungali wazi. Basi ewe Nabii wa rehema! Waambie hawa wapinzani kuwa wakikoma, wakaacha inadi yao na ushirikina wao, basi hapana shaka Mwenyezi Mungu atawasamehe vile vitendo vyao vilivyo kwisha pita. Na wakiendelea na upotovu wao, na wakarudia tena kukupigeni vita, basi mwendo wa Haki kwa walio tangulia umethibiti utakuwa ule ule, nao ni kuwa Haki lazima iushinde upotovu, pindi ikiwa wale watu wa Haki wakishika ut'iifu na njia za ushindi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wale waliokanusha upweke wa Allah Mtukufu miongoni mwa Washirikina wa watu wako kwamba ikiwa watakomeka na ukafiri na kumfanyia uadui Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na wakarudi kumuamini Allah Mtukufu Peke Yake na kutompiga vita Mtume na Waumini, Allah Mtukufu Atawasamehe madhambi yaliyopita, kwani Uislamu unafuta yaliyopita. Na watakaporudia washirikina hawa kukupiga vita baada ya tukio ambalo ulipata ushindi juu yao siku ya Badr, basi mwendo wa watu wa mwanzo umetangulia, nao ni kwamba wao wakikanusha na wakaendelea kwenye ukaidi wao, tutawaletea adhabu na mateso kwa haraka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net