Al-Anfaal 8:39
الأنفالوَقَـٰتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ ٱلدِّينُ كُلُّهُۥ لِلَّهِ ۚ فَإِنِ ٱنتَهَوْا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Na piganeni nao mpaka kusiwepo majaribio na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona vyema wanayayatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda. [39]
[39] Na endeleeni kuwapiga vita washirikina mpaka waache kuharibu itikadi za Waumini kwa kuwatesa na kuwaudhi. Wakiacha ukafiri na kuwaudhi Waumini, na wakamsafia Dini Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvijua vitendo vyao, na atawalipa kwavyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na piganeni na washirikina, enyi waumini, mpaka usiweko ushirikina na uzuiliaji wa njia ya Allah Mtukufu na kusiabudiwe isipokuwa Allah Mtukufu Peke Yake Asiye na mshirika, ili chuki ziwaondokee waja wa Allah Mtukufu katika ardhi na mpaka dini, utiifu na ibada vitakasiwe Allah Mtukufu tu bila mwingine. Wakiwa watakomeka na kuwafitini Waumini na kumshirikisha Allah Mtukufu na wakawa kwenye dini ya haki pamoja na nyinyi, basi Allah Mtukufu hakifichiki Kwake wanachokifanya cha kuacha ukafiri na kuingia kwenye Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net