Al-Anfaal 8:40
الأنفالوَإِن تَوَلَّوْا۟ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَوْلَىٰكُمْ ۚ نِعْمَ ٱلْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ ٱلنَّصِيرُ
Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema. [40]
[40] Na wakiendelea na kupuuza kwao na kuwaudhi Waumini, basi enyi Waumini, jueni ya kuwa nyinyi mko katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu, na huo ndio ulinzi wenye kupendeza na wenye nguvu kabisa. Na Yeye ndiye Mwenye kukunusuruni, na nusura yake ndio yenye nguvu zaidi na bora zaidi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wakiyapa mgongo hawa washirikina yale mliyowaitia, enyi Waumini, ya kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na kuacha kuwapiga vita nyinyi, na wakakataa isipokuwa kuendelea kwenye ukafiri na kuwapiga vita nyinyi, basi kuweni na yakini kwamba Allah Mtukufu ni Mwenye kuwasaidia na kuwapa ushindi juu yao. Yeye Ndiye bora wa kuwasaidia na kuwapa nyinyi ushindi na wale wenye kujitegemeza Kwake juu ya maadui zenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net