Al-Anfaal 8:41
الأنفالوَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَا غَنِمْتُم مِّن شَىْءٍ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُۥ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ إِن كُنتُمْ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا يَوْمَ ٱلْفُرْقَانِ يَوْمَ ٱلْتَقَى ٱلْجَمْعَانِ ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Na jueni ya kwamba ngawira yoyote mnayoipata, basi humusi yake ni ya Mwenyezi Mungu na ni ya Mtume, na ni ya jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mlimwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoyateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipokutana makundi yale mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. [41]
[41] Na enyi Waislamu! Jueni kuwa katika mali ya makafiri mliyo yateka, hukumu yake ni kugawiwa mafungu matano. Fungu moja ni la Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa zake Mtume, na mayatima, nao ni watoto wadogo wa Waislamu waliofiwa na baba zao nao ni mafakiri; na masikini, nao ni wale Waislamu wenye haja; na msafiri, naye ni mwenye kukatikiwa safari yake ya halali. Na yaliyo khusishwa katika hiyo sehemu moja katika tano kuwa ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume hukhusishwa kwa maslaha ya umma kama anavyo pasisha Mtume katika uhai wake, au, baada ya kufa kwake, Imam. Na yaliyo baki katika ile Khumsi watapewa walio kwisha tajwa. Ama sehemu nne nyengine katika ghanima (ngawira), na Aya ikanyamaza kimya juu yake, ni za wale walio pigana. Basi jueni hayo, na myajue ikiwa mmemuamini Mwenyezi Mungu kweli, na mmeziamini Ishara tulizo mteremshia mja wetu, Muhammad, za kumthibitisha na kumsaidia, siku ya Mpambanuo, tulipo pambanua baina ya ukafiri na Imani, nayo ndiyo siku lilipo kutana kundi lenu na kundi la makafiri katika Badri. Na Mwenyezi Mungu Mwenye kudra kubwa juu ya kila kitu aliwapa ushindi Waumini juu ya uchache wao, kuwashinda makafiri juu ya wingi wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na jueni, enyi Waumini, kwamba kile mlichokipata kutoka kwa adui yenu kupitia jihadi katika njia ya Allah Mtukufu, basi mafungu manne kati ya mafungu yake matano yapewe wapiganaji ambao walishiriki vitani, na fungu moja lililosalia kati ya yale mafungu matano litagawanywa sehemu tano: ya kwanza ni ya Allah Mtukufu na Mtume, iwekwe kwenye manufaa ya Waislamu wote; ya pili ni ya jamaa wa karibu na Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) nao ni waliozalikana na Hãshim na waliozalikana na Muṭṭalib.Wamewekewa sehemu hiyo ya tano mahali pa sadaka, kwani sadaka si halali kwao. Ya tatu ni ya mayatima; ya nne ni ya masikini, na ya tano ni ya msafiri aliyemalizikiwa na matumizi, iwapo nyinyi mnaukubali upweke wa Allah Mtukufu, mnamtii Yeye, ni wenye kuyaamini yale Aliyomteremshia mja Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) miongoni mwa ayah, usaidizi na ushindi katika siku Aliyopambanua baina ya haki na upotofu hapo Badr, siku lilipokutana kundi la Waumini na kundi la washirikina. Na Allah Mtukufu juu ya kila kitu ni Mwenye uwezo, Hashindwi na chochote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net