Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 42

Al-Anfaal 8:42

الأنفال

إِذْ أَنتُم بِٱلْعُدْوَةِ ٱلدُّنْيَا وَهُم بِٱلْعُدْوَةِ ٱلْقُصْوَىٰ وَٱلرَّكْبُ أَسْفَلَ مِنكُمْ ۚ وَلَوْ تَوَاعَدتُّمْ لَٱخْتَلَفْتُمْ فِى ٱلْمِيعَـٰدِ ۙ وَلَـٰكِن لِّيَقْضِىَ ٱللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا لِّيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عَنۢ بَيِّنَةٍ وَيَحْيَىٰ مَنْ حَىَّ عَنۢ بَيِّنَةٍ ۗ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ

Maana

Kumbukeni pale mlipokuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa kwenye ng'ambo ya mbali, na msafara ulipokuwa chini yenu. Na ingelikuwa mliagana, basi mngelihitilafiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo liliokuwa lazima litendwe. Ili aangamie wa kuangamia kwa ushahidi ulio wazi, na asalimike wa kusalimika kwa ushahidi ulio wazi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kumbukeni pale mlipo kuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa ng'ambo ya mbali, na msafara ulipo kuwa chini yenu. Na ingeli kuwa mmeagana mngeli khitalifiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lilio kuwa lazima litendeke, kwa sababu aangamie wa kuangamia kwa dalili zilizo dhaahiri, na asalimike wa kusalimika kwa dalili zilizo dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. [42]

[42] Na kumbukeni mlipo kuwa bondeni ng'ambo hii ya karibu na Madina, na wao makafiri wako ng'ambo ile ya mbali, na msafara wenye bidhaa mlio kuwa mnautaka uko karibu zaidi nanyi upande wa baharini. Na lau kuwa mmepeana miadi ya kukutana kwa kupigana basi msinge wafikiana hivyo. Lakini Mwenyezi Mungu kapanga mkutane bila ya miadi, na bila ya kutaka wao, ili apate kutekeleza jambo ambalo katika ujuzi wake limekwisha thibiti litokee tu, wala hapana jenginelo. Jambo lenyewe ni kuwa vitokee vita vitavyo pelekea nyinyi mshinde na wao washindwe. Ipate kuondoka shaka - wateketee wa kuteketea kwa hoja wazi ya kuonekana, nako ni kushindwa makafiri juu ya wingi wao; na wahuike Waumini kwa hoja iliyo wazi, nako ni kushinda kulio toka kwa Mwenyezi Mungu kuwapa Waumini wachache. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na kujua. Haimfichikii kauli wala niya yoyote ya pande zote mbili.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbukeni pindi mlipokuwa kwenye upande wa bonde lililokuwa karibu sana na mji wa Madina na maadui zenu wameshukia kwenye upande wa bonde la mbali, na msafara wa biashara upande wenu wa chini unaelekea kwenye ufuo wa Bahari Nyekundu. Na lau kama mungalijaribu kuweka maelewano ya makutano hayo mungalitafautiana, lakini Allah Mtukufu Aliwakusanya bila kuagana ili Alipitishe jambo ambalo ililazimu lifanyike kwa kuwaokoa vipenzi Vyake na kuwadhalilisha maadui Wake kwa kuuawa na kushikwa mateka. Na hili lilifanyika ili apate kuangamia mwenye kuangamia kati yao kutokamana na hoja ya Allah Mtukufu iliyomthibitikia akaiona na ikaondoa udhuru wake, na apate kuishi mwenye kuishi kutokamana na hoja ya Allah Mtukufu iliyomthibitikia na kujitokeza wazi kwake. Na kwa hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasikia maneno ya makundi mawili hayo, hakifichiki Kwake chochote, ni Mwenye kuzijua nia zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net