Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 43

Al-Anfaal 8:43

الأنفال

إِذْ يُرِيكَهُمُ ٱللَّهُ فِى مَنَامِكَ قَلِيلًا ۖ وَلَوْ أَرَىٰكَهُمْ كَثِيرًا لَّفَشِلْتُمْ وَلَتَنَـٰزَعْتُمْ فِى ٱلْأَمْرِ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ سَلَّمَ ۗ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Maana

Kumbuka Mwenyezi Mungu alipokuonyesha wao katika usingizi wako kwamba wao ni wachache, na lau angelikuonyesha kuwa ni wengi, basi mngeliingiwa na woga, na mngelizozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu akawapa salama. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyo vifuani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka alipo kuonyesha usingizini mwako kwamba wao ni wachache - na lau angeli kuonyesha kuwa ni wengi, mngeli ingiwa na woga, na mngeli zozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu kakuvueni. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua yalio vifuani. [43]

[43] Na kumbuka, ewe Mtume! Pale Mwenyezi Mungu alipo kufadhili kwa kukuonyesha usingizini ndoto ya kuwa hilo jeshi la maadui ni dogo, ili akutulizeni nyoyo muamini kuwa mtawashinda, kwa hivyo muwe imara kuwakaabili. Na lau angeli kuacheni muwaone wengi, bila ya kukuthibitisheni kwa ndoto hiyo, mngeli waogopa, na mkasita sita kupigana nao, na mngeli emewa, na mkazozana msonge mbele au mrudi. Lakini Mwenyezi Mungu amekuvueni na hayo, na akakuokoeni na matokeo yake, kwani hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo ndani ya vifua vya watu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Nabii, pindi Allah Mtukufu Alipokuonyesha uchache wa maadui zako ukiwa usingizini na ukawajulisha Waumini kuhusu hilo, ndipo nyoyo zao zikapata nguvu na wakawa na ujasiri wa kupigana nao. Na kama Anagalikuonyesha Mola wako wingi wa maadui zako, basi wangalisita Maswahaba wako kupambana nao, na mungalipatwa na uoga na mkatafautiana kuhusu kupigana, lakini Allah Mtukufu Aliepusha jambo la nyinyi kushindwa na Akaokoa na mwisho mbaya wa hilo. Hakika Yeye ni Mjuzi mno wa yaliyofichika nyoyoni na maumbile ya nafsi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net