Al-Anfaal 8:44
الأنفالوَإِذْ يُرِيكُمُوهُمْ إِذِ ٱلْتَقَيْتُمْ فِىٓ أَعْيُنِكُمْ قَلِيلًا وَيُقَلِّلُكُمْ فِىٓ أَعْيُنِهِمْ لِيَقْضِىَ ٱللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا ۗ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرْجَعُ ٱلْأُمُورُ
Na alipowaonyesha mlipokutana, katika macho yenu kuwa wao ni wachache, na akawafanya nyinyi ni wachache katika macho yao, ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lililokuwa lifanywe. Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mlipo kutana akakuonyesheni machoni mwenu kuwa wao ni wachache, na akakufanyeni nyinyi ni wachache machoni mwao, ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lilio kuwa liwe. Na mambo yote hurejezwa kwa Mwenyezi Mungu. [44]
[44] Na kumbuka, ewe Mtume! Alipo kuonyeshemi Mwenyezi Mungu kuwa maadui zenu mnapo kutatana nao ni wachache katika macho yenu, kama alivyo waonyesha wao kuwa nyinyi ni wachache, na kwa kuwa tangu hapo wao wana ghururi ndani ya nafsi zao kuwa ni wengi, ili kila mmoja wenu awanie kupigana na mwenzie, na kwa hivyo yatimie aliyo kwisha yaamrisha Mwenyezi Mungu. Na ilikuwa hapana budi hayo yatimie. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio hurejea mambo yote ya ulimwengu. Halitendeki jambo ila alilo kwisha lihukumia na kuzitengeneza sababu zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka pia pindi walipojitokeza maadui kwenye ardhi ya mapigano mkawaona kuwa ni wachache mkawa na ujasiri juu yao, na Akawafanya nyinyi ni wachache kwenye macho yao, ili waache kujiandaa kupigana na nyinyi, ili Allah Mtukufu Alipitishe jambo ambalo hapana budi lifanyike, ili itimie ahadi ya Allah Mtukufu kwenu ya himaya na ushindi. Hapo likawa neno la Allah Mtukufu ndilo la juu, na neno la wale waliokanusha ndilo la chini. Na kwa Allah Mtukufu ndiko marudio ya mambo yote, Apate kumlipa kila mmoja kwa anachostahili kulipwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net