Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 45

Al-Anfaal 8:45

الأنفال

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَٱثْبُتُوا۟ وَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Mkikutana na kikundi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mfaulu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa. [45]

[45] Enyi mlio amini! Mkikutana na kikosi cha wapiganaji katika adui zenu, basi kuweni imara, wala msiwakimbie. Na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa kufuata uwezo wake, na ahadi yake ya kuwasaidia Waumini, mkikithirisha kumkumbuka na kumtaja pamoja na kuwa imara na kusubiri. Mkifanya hivyo ndio matarajio yenu ya kupata mafanikio yatapo timia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, mkutanapo na kundi la watu wa ukafiri wakawa wamejitayarisha kupigana na nyinyi, basi thibitini na msishindwe na wao na mumtaje Allah Mtukufu kwa wingi, hali ya kuomba na kunyenyekea, Awateremshie ushindi na uwezo wa kumshinda adui yenu, ili mfaulu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net