Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 12

Al-Anfaal 8:12

الأنفال

إِذْ يُوحِى رَبُّكَ إِلَى ٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ أَنِّى مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا۟ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۚ سَأُلْقِى فِى قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلرُّعْبَ فَٱضْرِبُوا۟ فَوْقَ ٱلْأَعْنَاقِ وَٱضْرِبُوا۟ مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ

Maana

Mola wako Mlezi alipowafunulia Malaika: Hakika Mimi niko pamoja nanyi, basi watieni nguvu wale walioamini. Nitatupa woga katika nyoyo za wale waliokufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wako Mlezi alipo wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu walio amini. Nitatia woga katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole. [12]

[12] Enyi Waumini! Kumbukeni pale Mwenyezi Mungu alipo wafunulia wale wenye Roho zilio t'ahirika, yaani Malaika, watie ndani ya nyoyo zenu kuwa Mimi ni pamoja nanyi, nakuungeni mkono, na ninakusaidieni, kwa kuwaambia: Zitieni nguvu nyoyo za walio amini, wait'ii Haki na wapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mimi nitaifanya khofu izitawale nyoyo za washirikina, nao watakuogopeni. Nanyi enyi Waumini! Wapigeni vichwani mwao vilio juu ya shingo zao, na kateni vidole vyao vinavyo kamata panga.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka pindi Mola wako, ewe Nabii, Alipowapelekea wahyi Malaika ambao Allah Mtukufu Aliwasaidia nao Waislamu katika vita vya Badr, «Mimi nipo na nyinyi, nawasaidia na kuwahami, watieni hima wale walioamini, nitaweka kwenye nyoyo za waliokanusha kicho kingi, unyonge na utwevu.» Vipigeni, enyi Waumini, vichwa vya makafiri na wapigeni wao kila ncha na kila kiungo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net