Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 13

Al-Anfaal 8:13

الأنفال

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَآقُّوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ ۚ وَمَن يُشَاقِقِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Maana

Hayo ni kwa sababu walimuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu wamemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. [13]

[13] Ukawa ushindi na kuungwa mkono nyinyi, na kwao ni kitisho na fazaa, kwani wao walikuwa upande mmoja, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake walikuwa upande mwengine, kwa kuwa wao walimpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi ndio Mwenyezi Mungu anawateremshia adhabu chungu. Na adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hayo yaliyojiri ya kuwapiga makafiri vichwa vyao, shingo zao na ncha zao ni kwa kuwa wao walienda kinyume na amri ya Allah Mtukufu na Mtume Wake. Na yoyote mwenye kwenda kinyume cha amri ya Allah Mtukufu na Mtume Wake, basi Allah Mtukufu ni Mkali wa mateso kwake ulimwenguni na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net