Al-Anfaal 8:14
الأنفالذَٰلِكُمْ فَذُوقُوهُ وَأَنَّ لِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابَ ٱلنَّارِ
Ndivyo hivyo! Basi ionjeni! Na bila ya shaka makafiri wana adhabu ya Moto.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ndio hivyo! Basi ionjeni! Na bila ya shaka makafiri wana adhabu ya Moto. [14]
[14] Enyi Waumini! Hivyo ndio vita, basi vionjeni, na muwe na yakini kuwa mtapata nusura na kuungwa mkono. Na wanao pinga Ishara za Mwenyezi Mungu watapata adhabu nyengine Siku ya Kiyama, nayo ni adhabu ya Moto.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Adhabu hiyo niliyoiharakisha kwenu, enyi makafiri mnaoenda kinyume na amri za Allah Mtukufu ulimwenguni, ionjeni katika maisha ya kilimwengu, na huko Akhera mtakuwa na adhabu ya Moto.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net