Al-Anfaal 8:15
الأنفاليَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ ٱلْأَدْبَارَ
Enyi Mlioamini! Mnapokutana na wale waliokufuru vitani, msiwageuzie migongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru vitani msiwageuzie mgongo. [15]
[15] Enyi mlio isadiki Haki na mkait'ii! Mkikutana na wale walio kufuru katika uwanja wa vita nao wanakujieni kwa wingi wao, msiwakimbie mkazipa mgongo panga zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi wale ambao mmemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafuata sheria Yake kivitendo, mpambanapo na waliokanusha katika vita wakawa wanasogea karibu yenu msiwape migongo yenu na mkakubali kushindwa na wao, lakini kuweni imara na wao, kwani Allah Mtukufu yuko pamoja na nyinyi na ni Mwenye kuwapa ushindi juu yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net