Al-Anfaal 8:16
الأنفالوَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُۥٓ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٍ فَقَدْ بَآءَ بِغَضَبٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَمَأْوَىٰهُ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ
Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo, isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi, basi hakika atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahali pake ni Jahannam, na hayo ndiyo marejeo mabaya kabisa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu. [16]
[16] Na asiye wakaabili uso kwa uso, basi Mwenyezi Mungu amekasirika naye, na marejeo yake ni Motoni. Na huo ndio mwisho muovu kweli. Na mwenye kuacha kuwakaabili kwa kuwa ni hila na mbinu za vita, au kaacha kikosi kwenda jiunga na kikosi kingine cha Waumini apate kuwa na nguvu zaidi za mpambano, huyo hana dhambi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yoyote katika nyinyi atawapa mgongo wake kwenye vita, isipokuwa kwa kupenya kama mbinu ya vita ya kuwachimba makafiri au kujiunga na mjumuiko wa waislamu walio vitani popote walipo, basi huyo amestahili kukasirikiwa na Allah Mtukufu, na makao yake ni Moto wa Jahanamu ambao ni mahali pabaya sana pa kuishia na kukomea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net