Al-Anfaal 8:17
الأنفالفَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ رَمَىٰ ۚ وَلِيُبْلِىَ ٱلْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَآءً حَسَنًا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Kwa hivyo, hamkuwaua nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua. Nawe hukutupa ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa, na ili awajaribu Waumini majaribio mazuri kutoka kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hamkuwauwa nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye wauwa. Na wewe hukutupa, walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye tupa, ili awajaribu Waumini majaribio mema yatokayo kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Msikizi na Mjuzi. [17]
[17] Na nyinyi Waumini, pale mnapo washinda, na mkawauwa mlio wauwa katika wao, basi hakika si nyinyi mlio wauwa kwa nguvu zenu, lakini ni Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliye kupeni ushindi na kuweza kuwauwa, kwa msaada wake kwenu na kutia khofu katika nyoyo zao. Na wewe Mtume, pale ulipo warushia mchanga na kokoto nyusoni mwao kuwafazaisha, si wewe ulio rusha, lakini ni Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliye rusha, na wao wakafazaika. Na hayo Mwenyezi Mungu ameyafanya kuwaneemesha Waumini kwa neema njema. Katika hayo pana majaribio ya nguvu kwao, ili ionekane ikhlasi yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mambo yao, Mwenye kusikia maneno yao, na Mwenye kujua mambo ya maadui zao na kauli zao pia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nyinyi, enyi Waumini, hamkuwauwa washirikina siku ya Badr, lakini Allah Mtukufu ndiye Aliwaua, kwa kuwa Aliwasaidia nyinyi kufanya hilo. Na hukurusha uliporusha, ewe Nabii, lakini ni Allah Mtukufu Aliyerusha, kwa kuwa Alikifikisha kile ulichokirusha kwenye nyuso za washirikina; na ili Allah Mtukufu Awafanyie mtihani wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, na Awafikishe kwa sababu ya jihadi kwenye daraja za juu, na Awajulisha wao neema Zake kwao wapate kumshukuru, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa hilo. Hakika Allah Mtukufu ni Msikizi wa dua zenu na maneno yenu mliyoyaficha na mliyoyafanya waziwazi, ni Mjuzi wa yenye nafuu kwa waja Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net