Al-Anfaal 8:18
الأنفالذَٰلِكُمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُوهِنُ كَيْدِ ٱلْكَـٰفِرِينَ
Hayo! Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha njama za makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ndio hivyo! Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha vitimbi vya makafiri. [18]
[18] Huo ndio ushindi mkubwa, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kudhoofisha kila hila za makafiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kitendo hiki cha kuwaua washirikina na kuwarushia waliposhindwa na mtihani mzuri wa kuwapa ushindi Waumini juu ya maadui zao, huo unatoka kwa Allah Mtukufu kuja kwa Waumini, na kwamba Allah Mtukufu, mbeleni, ni mwenye kuvikosesha nguvu na kuvimaliza vitimbi vya makafiri mpaka wawe wanyonge na wafuate haki au waangamie.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net