Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 19

Al-Anfaal 8:19

الأنفال

إِن تَسْتَفْتِحُوا۟ فَقَدْ جَآءَكُمُ ٱلْفَتْحُ ۖ وَإِن تَنتَهُوا۟ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَعُودُوا۟ نَعُدْ وَلَن تُغْنِىَ عَنكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْـًٔا وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Mkiomba msaada wa ushindi, basi msaada wa ushindi ulikwishawajia. Na mkikomeka, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkirejea, Sisi pia tutarejea. Na kundi lenu halitawanufaisha kitu hata kama yatakuwa (makundi) mengi. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kama mnataka hukumu basi hukumu imekwisha kujieni. Na mkiacha itakuwa ndio kheri kwenu. Na mkirejea Sisi pia tutarejea. Na jeshi lenu halitakufaeni kitu, japo likiwa kubwa. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini. [19]

[19] Ikiwa nyinyi washirikina mlikuwa mkining'inia mapazia ya Al Kaaba na huku mnaomba yapambanuliwe baina yenu na Waumini ijuulikane haki ipo wapi, basi sasa imekwisha kujieni hukumu ya kupambanua, na ushindi si wenu, bali ni wa Waumini. Na nyinyi mkirejea tena kufanya uadui Nasi tutakushindeni tena. Wala kukusanyika kwenu kwa ajili ya madhambi hakutakufaeni kitu! Hata ikiwa idadi yenu kubwa vipi! Kwani hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao isaidiki Haki na wanaikubali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Muombapo, enyi makafiri, kwa Allah Mtukufu Ayalete mateso na adhabu Yake kwa wale wenye kupita mipaka na kudhulumu, basi Allah Mtukufu Ameshaitikia maombi yenu Alipowaletea mateso Yake yaliyokuwa ni adhabu kwenu na ni mazingatio kwa wacha Mungu.Na iwapo mtakomeka, enyi makafiri, kumkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake na kumpiga vita Nabii wake (sala na salamu zimuendee) hilo ni bora kwenu katika ulimwengu wenu na Akhera yenu. Na mkirudi vitani na kumpiga vita Muhammad, (sala na salamu zimuendee) na kuwapiga vita wafuasi wake Waumini, basi tutarudia kuwashinda kama mlivyoshindwa Siku ya Badr. Na hautawafaa mkusanyiko wenu kitu chochote kama ambavyo haukuwafaa siku ya Badr, pamoja na wingi wa idadi yenu na zana zenu na uchache wa idadi ya waumini na zana zao. Na Allah Mtukufu yuko pamoja na Waumini kwa kuwasaidia na kuwapa ushindi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net