Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 20

Al-Anfaal 8:20

الأنفال

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَوَلَّوْا۟ عَنْهُ وَأَنتُمْ تَسْمَعُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msigeuke mkamuacha hali ya kuwa mnasikia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msijiepushe naye, nanyi mnasikia. [20]

[20] Enyi mlio isadiki Haki, na mkaifuata! Hakika mmejua ushindi umepatikana kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kumt'ii Mtume wake. Basi endeleeni kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume. Wala msiupuuze wito wa Mtume anao itia Haki, nanyi mnamsikia na mnafahamu ayasemayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mmemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, kuweni na utiifu kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake katika yale Aliyowaamrisha kwayo na Akawakataza nayo, na msiache kumtii Allah Mtukufu na kumtii Mtume Wake na hali nyinyi mnazisikia hoja na dalili zinazosomwa kwenu kwenye Qur’ani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net