Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 21

Al-Anfaal 8:21

الأنفال

وَلَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّذِينَ قَالُوا۟ سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ

Maana

Wala msiwe kama wale wanaosema, "Tumesikia" na hali hawasikii.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msiwe kama wale wanao sema: Tumesikia, na kumbe hawasikii. [21]

[21] Wala msiwe kama wanaafiki wanao sema: Tumeisikia Haki na tumefahamu. Lakini hawaifuati wala hawaiamini. Basi wamekuwa kama wasio sikia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala msiwe, enyi Waumini, katika kwenda kinyume kwenu na Allah Mtukufu na Mtume Wake, (sala na salamu zimuendee) ni kama washirikina na wanafiki ambao wakisikia Kitabu cha Allah Mtukufu kinasomwa kwao huwa wakisema, «Tumesikia kwa masikio yetu,» na hali wao kwa hakika hawayazingatii wanayoyasikia wala hawayatii akilini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net