Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 22

Al-Anfaal 8:22

الأنفال

إِنَّ شَرَّ ٱلدَّوَآبِّ عِندَ ٱللَّهِ ٱلصُّمُّ ٱلْبُكْمُ ٱلَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ

Maana

Hakika waovu mno wa wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale viziwi, na mabubu wasiotumia akili zao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni vile viziwi na bubu visio tumia akili zao. [22]

[22] Hao washirikina na wanaafiki ni kama wanyama waovu kabisa walio sibiwa na uziwi, kwa hivyo hawasikii; na wakasibiwa na ububu, kwa hivyo hawasemi. Basi wao ni viziwi kwa Haki, na hivyo hawasikii, wala hawaitamki na hawaielewi!!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika waovu zaidi wa wanaotembea kwenye ardhi, miongoni mwa viumbe vya Allah Mtukufu, mbele ya Allah Mtukufu ni viziwi ambao masikio yao yameziba kutoisikia haki wakawa hawasikii, mabubu ambao ndimi zao zimeshikwa kutoitamka haki wakawa hawatamki. Hawa ndio wale wasioelewa maamrisho na makatazo yanayotoka kwa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net