Al-Anfaal 8:23
الأنفالوَلَوْ عَلِمَ ٱللَّهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَّأَسْمَعَهُمْ ۖ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ لَتَوَلَّوا۟ وَّهُم مُّعْرِضُونَ
Na Mwenyezi Mungu angelijua heri yoyote ndani yao, angewasikilizisha, na lau angewasikilizisha, wangeligeuka hali ya kuwa wamepuuza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu angeli jua wema wowote kwao ange wasikilizisha, na lau ange wasikilizisha wangeli geuka wakapuuza. [23]
[23] Na Mwenyezi Mungu kwa ilimu yake ya tangu na tangu lau angeli ona ndani yao kuwa, katika hali yao hivi sasa, itakuja patikana kheri yoyote kwao hao kwa nafsi zao, na kwa watu, na kwa Haki, basi angeli wafanya wasikie kusikia kwa kuongoka hata Haki ikaingia akilini mwao. Na hata wangeli isikia na wakaifahamu Haki basi bado wasingeli ifuata. Na mapuuza hayawaachi kwa kuzidiwa na pumbao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau Allah Mtukufu angejua kwamba ndani ya hawa kuna kheri yoyote Angaliwafanya wasikie mawaidha ya Qur’ani na mazingatio yake mpaka wazifahamu hoja na dalili za Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka. Lakini Yeye Alijua kwamba hamna kheri kwao na kwamba wao hawataamini. Na lau Aliwasikilizisha, kwa kukadiria na kukisia, wangaliipa mgongo Imani kwa kusudi na ujeuri, baada kuielewa. Na wao ni wenye kuipa mgongo, hawazunguki kuitazama haki kwa njia yoyote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net