Al-Anfaal 8:24
الأنفاليَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَجِيبُوا۟ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ ٱلْمَرْءِ وَقَلْبِهِۦ وَأَنَّهُۥٓ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaitia yale yenye kuwahuisha. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huzuia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye mtakusanywa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa. [24]
[24] Enyi mlio isadiki Haki na mkaifuata! Muitikieni Mwenyezi Mungu kwa kufikisha anayo kuamrisheni. Na muitikieni Mtume katika vile anavyo fikisha anayo yaamrisha Mwenyezi Mungu, pale anapo kuiteni Mtume kufuata amri za Mwenyezi Mungu ambazo zitakuleteeni uzima wa miili yenu, na roho zenu, na akili zenu, na nyoyo zenu. Na mjue kwa yakini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenya kuangalia nyoyo zenu. Huzielekeza atakavyo. Basi Yeye huingilia baina yenu na nyoyo zenu zinapo ingiliwa na matamanio, Yeye basi hukuokoeni nayo ikiwa nyinyi wenyewe mnajielekeza kwenye Njia iliyo nyooka. Na nyinyi nyote mtakusanywa kwake Siku ya Kiyama, na huko ndiko malipo yatakuwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi ambao mmemuamini Allah Mtukufu kuwa ni Mola na Muhammad kuwa ni Nabii na ni Mtume, Itikieni mwito wa Allah Mtukufu na wa Mtume kwa kumtii awaitapo kwenye haki yenye kuwapa uhai. Kwani katika kuitikia mwito huo kunatengeneza maisha yenu katika ulimwengu na Akhera. Na mjue, enyi Waumini, kwamba Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Mwenye kuendesha kila kitu na Ndiye Muweza, Anaingilia kati baina ya mtu na kile ambacho moyo wake unakitamani. Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayestahiki kuitikiwa Akiwaita, kwani mamlaka ya kila kitu yako mkononi Mwake. Na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwa Siku isiyo na shaka, ambapo kila mmoja atalipwa kwa analostahili kulipwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net