Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 11

Al-Anfaal 8:11

الأنفال

إِذْ يُغَشِّيكُمُ ٱلنُّعَاسَ أَمَنَةً مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِۦ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ ٱلشَّيْطَـٰنِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ ٱلْأَقْدَامَ

Maana

Alipowafunika kwa usingizi uwe ni amani kutoka kwake, na akawateremshia maji kutoka mbinguni ili awasafishe kwayo na awaondolee uchafu wa Shetani, na ili azifunge nyoyo zenu, na aimarishe kwayo miguu yenu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alipo kufunikeni kwa usingizi uwe ni uaminisho kutoka kwake, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo na kukuondoleeni uchafu wa Shet'ani, na kuzipa nguvu nyoyo zenu, na kuitia imara miguu yenu. [11]

[11] Enyi Waumini! Kumbukeni wakati mlipo ingiwa khofu kwa upungufu wa maji, na kuwaogopa maadui. Mwenyezi Mungu alikupeni utulivu, kwa kukuleteeni usingizi, mkalala mkatua. Akakuteremshieni maji kutoka mbinguni mkajisafishia, na mkauondoa wasiwasi wa Shetani, na nyoyo zenu zikawa imara kwa msaada wa Rahmani na pia ardhi ikashikamana kwa hayo maji, na miguu yenu ikaweza kukanyaga bila ya kudidimia katika mchanga. Aya hii inaashiria fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya wapiganaji Waumini kwa kupatikana hali ya amani kwa kupumzika kwa usingizi, na kuteremka mvua kwa kujitahirisha na kukoga, na kushikamana mchanga kwa kuwepo maji, basi nyayo zikasimama imara. Inajuulikana kuwa mchanga laini unawaletea taabu wapiganaji na unakuwa pingamizi katika kwenda huku na huko ambako ni katika dharura za vita muhimu. Na aya ya pili inaeleza maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwaambia Malaika wawathibitishe Waumini na watie khofu katika nyoyo za makafiri. Na ni maarufu kuwa khofu ikiwatawala askari katika midani huwaletea kuemewa. Na katika Aya hii tukufu panaashiriwa pahali pa kupiga napo ni juu ya shingo na kuvikata vidole vinavyo kamata silaha mkononi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbukeni pindi Allah Mtukufu Alipowatia usingizi, ili kuwapa hisia ya amani ya kutoogopa kwamba adui yenu atawashinda, na kuwateremshia kutoka mawinguni maji safi, ili mjisafishe kwayo na uchafu wa nje na Awaondolee ndani wasiwasi na mawazo yanayoletwa na Shetani, na ili Aziimarishe nyoyo zenu kwa kuvumilia kwenye vita, na ili nyayo za Waumini ziwe thabiti zisiteleze kwa kuifanya ngumu ardhi ya mchanga kwa mvua hiyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net