Al-Anfaal 8:10
الأنفالوَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشْرَىٰ وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِۦ قُلُوبُكُمْ ۚ وَمَا ٱلنَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Na Mwenyezi Mungu hakufanya hayo isipokuwa yawe ni bishara na ili nyoyo zenu zitue kwayo. Na nusura haiwi isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zituwe. Na haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima. [10]
[10] Wala Mwenyezi Mungu Mtukufu hakujaalia huko kukuungeni mkono kwa (Malaika) hizo Roho safi ila ni kuwa ni kukupeni khabari njema, kama bishara kwenu kuwa mtashinda, mpate kutua nyoyo na msonge mbele. Na Mwenyezi Mungu anakusaidieni, na wala ushindi hauji ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye kushinda, ambaye anaye panga mambo kwa pahala pake kwa mujibu wa ujuzi wake usio pitikiwa na chochote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Hakuufanya msaada huo isipokuwa ni bishara kwenu ya ushindi na ili nyoyo zenu zitulie na muwe na yakini ya kupata ushindi kutoka kwa Allah Mtukufu, kwani ushindi watoka kwa Allah Mtukufu tu, si kwa ukali wa zana zenu na nguvu zenu. Hakika Allah Mtukufu ni Mshindi katika ufalme Wake ni Mwenye hekima katika upelekeshaji Wake na uwekaji sheria Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net