Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 9

Al-Anfaal 8:9

الأنفال

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَٱسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّى مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ مُرْدِفِينَ

Maana

Mlipokuwa mnamuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akawaitikia kuwa Mimi hakika nitawasaidia kwa elfu moja miongoni mwa Malaika wakifuatana mfululizo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akakujibuni kuwa: Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu wanao fuatana mfululizo. [9]

[9] Na enyi Waumini! Kumbukeni nanyi mnagawana ngawira na mnakhitalifiana, mlipo omba uwokovu na msaada, na mkaandikiwa kuwa hapana la kukuepusheni na vita. Mwenyezi Mungu alikuitikieni maombi yenu, akakuungeni mkono kwa kukuleteeni (Malaika) Roho zilizo safi nyingi zinazo fika elfu zinazo fuatana, zikija moja baada ya moja. Walipo jua wapiganaji Waumini kuwa hapana njia ya kuepukana na vita wakaomba msaada kwa Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaitikia, na akawaunga mkono kwa Malaika elfu walio fuatana. Yaani alianza kwa kupeleka msaada kwa vikosi vilivyo fuatana ili iwe wepesi kwa kila kikosi kuelekea pahala pake katika vita pasiwepo kukaa bure au kupigana makumbo. Na ifikapo misaada ya majeshi ya vita roho hufurahi na moyo huingia nguvu. Na hayo ndiyo aliyo yakusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kauli yake: "Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zituwe." Na ushindi daima unatokana na Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbukeni neema ya Allah Mtukufu kwenu siku ya Badr mlipoomba mpate ushindi juu ya adui yenu, Allah Mtukufu Akakubali maombi yenu kwa kusema, «Mimi nitawasaidia kwa Malaika elfu moja kutoka mbinguni wakifuatana hawa baada ya wengine».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net