Al-A'raaf 7:33
الأعرافقُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّىَ ٱلْفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلْإِثْمَ وَٱلْبَغْىَ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا۟ بِٱللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِۦ سُلْطَـٰنًا وَأَن تَقُولُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
Sema: Hakika Mola wangu Mlezi ameharamisha machafu, yaliyodhihiri yake na ya siri, na dhambi, na kuvuka mipaka bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na ambacho hakukiteremshia uthibitisho wowote, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua. [33]
[33] Ewe Muhammad! Sema: Hakika Mola wangu Mlezi ameharimisha mambo yaliyo zidi kwa ubaya, kama uzinzi; sawa sawa ukifanywa kwa siri au kwa dhaahiri. Pia ameharimisha kila maasi ya namna yoyote, na dhulma isiyo na njia ya haki. Na ameharimisha kumshirikisha na chochote kisicho kuwa na hoja madhubuti, au dalili ya kweli. Na pia kumzulia uwongo Subhanahu, Aliye takasika, katika kuhalalisha na kuharimisha, na mengineyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema,ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Hakika Allah Mtukufu Ndiye Aliyeyafanya matendo maovu kuwa ni haramu, yale yaliyo waziwazi na yale yaliyofichika, na Ameyakataza maasia yote, na miongoni mwa makubwa zaidi ya maasia ni kuwafanyia watu uadui, kwani hilo liko kando na haki. Na Amewaharamishia kuabudu, pamoja na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, vitu vyingine kati ya vile ambavyo Hakuviteremshia ushahidi wala hoja, kwani afanyaye hayo hana kithibitisho chochote. Na Amewaharamishia kumnasibishia Allah Mtukufu, Aliyetukuka, sheria ambayo Hakuipasisha kwa kumzulia urongo,» kama madai ya kwamba Allah Mtukufu Ana mwana na kuharamisha baadhi ya vilivyo halali katika mavazi na chakula.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net