Al-A'raaf 7:34
الأعرافوَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ
Na kila umma una muda wake. Na unapokuja muda wao, basi hawakawii hata saa moja, wala hawatangulii.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kila umma una muda wake. Utakapo fika muda wao basi hawatakawia hata saa moja, wala hawatatangulia. [34]
[34] Na kila umma una ukomo wake maalumu. Na hapana uwezo wowote wa kuupeleka mbele mwisho huo au kuuakhirisha muda wake hata ukiwa mdogo vipi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kila kikundi kilichojikusanya kumkanusha Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na kuwakanusha Mitume Wake, amani iwashukie, kina wakati wa kushukiwa na mateso. Huo wakati, Aliouweka Allah Mtukufu wa kuwaangamiza, hawatakawia nao, japokuwa kwa muda mfupi, wala hawatautangulia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net