Al-A'raaf 7:35
الأعرافيَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ ءَايَـٰتِى ۙ فَمَنِ ٱتَّقَىٰ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Enyi wanadamu! Watakapowajia Mitume miongoni mwenu wakiwasimulia Ishara zangu, basi mwenye kumcha Mungu na akatengenea, haitakuwa hofu kwao, wala wao hawatahuzunika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi wanaadamu! Watakapo kufikieni Mitume miongoni mwenu wakakuelezeni Ishara zangu, basi watakao mchamngu na wakatengenea haitakuwa khofu kwao, wala hawatahuzunika. [35]
[35] Enyi wanaadamu! Wakikujieni Mitume kutokana na hiyo jinsi yenu ya kibinaadamu kukufikishieni Ishara zangu zilizo funuliwa nyinyi mnakuwa makundi mawili. Kwa wale wenye kuamini na wakatenda mema kwa usafi wa niya, hapana khofu, wala wao hawatahuzunika katika dunia yao na Akhera yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi wanadamu! Pindi watakapokuja kwenu Mitume wangu, miongoni mwa watu wenu, wakiwasomea aya za Kitabu changu na kuwafahamisha hoja juu ya ukweli wa yale waliyokuja nayo, basi watiini, kwani mwenye kujikinga na hasira zangu na akayatengeneza matendo yake, hao hawatakuwa na hofu na mateso ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama wala hawatahuzunika juu yale yaliyowapita miongoni mwa hadhi za duniani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net