Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 32

Al-A'raaf 7:32

الأعراف

قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ ٱللَّهِ ٱلَّتِىٓ أَخْرَجَ لِعِبَادِهِۦ وَٱلطَّيِّبَـٰتِ مِنَ ٱلرِّزْقِ ۚ قُلْ هِىَ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ

Maana

Sema: Ni nani aliyeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu alilowatolea waja wake, na vile vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa wale walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivyo ndivyo tunavyowaelezea Ishara kaumu wanaojua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua. [32]

[32] Ewe Muhammad! Waambie kwa kuupinga ule uzushi wao kumzulia Mwenyezi Mungu juu ya kuhalalisha na kuharimisha: Nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo waumbia waja wake? Na nani aliye harimisha riziki iliyo halali na nzuri? Waambie: Hivi vitu vizuri ni neema inayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Isingeli faa wastarehe navyo duniani ila wale walio amini, kwa sababu wao wanatimiza haki yao kwa shukrani na ut'iifu. Lakini rehema ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu, imewakusanya pia makafiri na wakhalifu katika dunia. Na Siku ya Kiama neema hizi zitakuwa za Waumini peke yao, wala hapana mwenginewe ataye shirikiana nao katika hayo. Na Sisi tunazieleza Aya, Ishara, zinazo onyesha hukumu kwa mpango huu ulio wazi kwa ajili ya watu wanao fahamu kwamba hakika Mwenyezi Mungu peke yake, Mwenye kumiliki kila kitu, ndiye Mwenye uwezo wa kuhalalisha na kuharimisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, uwaambie hao wajinga miongoni mwa washirikina, «Ni nani aliyewaharamishia vazi zuri ambalo Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Amelifanya kuwa ni pambo kwenu? Na ni nani Aliyewaharamishia kujistarehesha kwa chakula kizuri cha halali kilichoruzukiwa na Allah Mtukufu?» Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina, Kwa hakika vile alivyoviruhusu Allah Mtukufu, miongoni mwa mavazi na vitu vizuri miongoni mwa vyakula na vinywaji, ni haki kwa walioamini pamoja na wengineo katika maisha ya ulimwenguni, na ni haki kwa walioamini peke yao Siku ya Kiyama. Maelezo kama hayo ni mafundisho ambayo Allah Mtukufu Anayaelezea kwa watu wenye kuyajua mambo wanayoelezwa na kuyaelewa wanayofafanuliwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net