Al-A'raaf 7:31
الأعرافيَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ خُذُوا۟ زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ وَلَا تُسْرِفُوٓا۟ ۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلْمُسْرِفِينَ
Enyi wanadamu! Chukueni pambo lenu mnapokwenda kwenye kila mahali pa kusudjudu (kama vile msikiti), na kuleni, na kunyweni, wala msipitilize. Kwa hakika Yeye hapendi wanaopitiliza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu. [31]
[31] Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu, nalo ni nguo hizi "maaddiy" za kuonekana, za kusitiri utupu, na nguo za "adabiy" zisizo onekana, bali ni za maana, nazo ni Taqwa, Uchamngu, katika kila pahala pa Swala, na kila wakati mnapo fanya ibada. Na jistarehesheni kwa kula na kunywa bila ya kufanya israfu au ubadhirifu, yaani kutumia kwa fujo, katika hayo. Basi msitumie vitu vilivyo harimishwa, wala msipite kiasi cha kiakili katika huko kujistarehesha. Hakika Mwenyezi Mungu hana radhi na wanao tumia kwa fujo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi wanadamu! Kuweni, kila mnapotekeleza Swala, katika hali ya pambo linalokubalika kisheria la nguo zinazofinika tupu zenu na muwe katika hali ya usafi, utohara na mfano wake. Na kuleni na kunyweni katika vizuri Alivyowapa Allah Mtukufu, wala msikiuke mipaka ya wastani, kwani Allah Mtukufu Hawapendi wakiukaji wenye kupitisha kiasi katika vyakula na vinywaji na mengineyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net