Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 30

Al-A'raaf 7:30

الأعراف

فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيْهِمُ ٱلضَّلَـٰلَةُ ۗ إِنَّهُمُ ٱتَّخَذُوا۟ ٱلشَّيَـٰطِينَ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ

Maana

Kundi moja ameliongoa, na kundi jingine limethibitikiwa na upotovu. Kwa hakika hao waliwafanya mashetani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao wameongoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hali ya kuwa kundi moja amelihidi, na kundi jengine limethibitikiwa na upotofu. Kwa hakika hao waliwafanya mashet'ani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao wameongoka. [30]

[30] Siku ya Kiyama watu watakuwa makundi mawili:- Kundi moja lilio pata tawfiqi ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa lilichagua Njia ya Haki, likaamini na likatenda vitendo vyema. Na kundi jengine limehukumiwa upotovu, kwa sababu lilikhiari njia ya baat'ili, nayo ni ukafiri na uasi! Na hao walio potea waliwafanya mashetani ndio rafiki zao badala ya Mwenyezi Mungu, wakawafuata, nao wanadhani kuwa wao wamewafikiwa kwa kudanganyika kwao na khadaa za mashetani!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Amewafanya waja wake makundi mawili: kundi moja Amelielekeza kwenye uongofu, kwenye njia iliyolingana; na kundi lingine limelazimika kupotea njia iliyolingana, kwani wao wamewafanya Mashetani ni wategemewa wao badala ya Allah Mtukufu, waliwasikiliza Mashetani kwa ujinga wao na kudhania kwao kuwa wao wamefuata njia ya uongofu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net