Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 203

Al-A'raaf 7:203

الأعراف

وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِم بِـَٔايَةٍ قَالُوا۟ لَوْلَا ٱجْتَبَيْتَهَا ۚ قُلْ إِنَّمَآ أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ مِن رَّبِّى ۚ هَـٰذَا بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Maana

Na usipowajia na Ishara, wanasema: Kwa nini hukuibuni? Sema: hakika mimi ninafuata tu yale yanayofunuliwa kwangu kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Hii (Qur'ani) ni hoja zinazotoka kwa Mola wenu Mlezi, na uongofu, na rehema kwa kaumu wanaoamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na usipo waletea Ishara waitakayo husema: Kwa nini hukuibuni? Sema: mimi ninafuata yanayo funuliwa kwangu kutokana na Mola Mlezi wangu. Hii (Qur'ani) ni hoja zinazo toka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu na rehema kwa watu wanao amini. [203]

[203] Na usipo waletea makafiri Ishara wanayo itaka kwa inadi na ukafiri, husema: Kwa nini hukuitaka? (au hukuizua? Makusudio yao ni kuwa Mtume s.a.w. akizibuni Aya zote.) Waambie: Mimi sifuati ila Qur'ani ninayo funuliwa kwa wahyi kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Na waambie: Hii Qur'ani ni hoja zinazo toka kwa Mola Mlezi wenu kukuonyesheni njia za Haki. Nayo ina uwongofu, na rehema, kwa Waumini, kwa sababu wao wanaifuata kwa vitendo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na usipowajia, ewe Mtume, washirikina hawa na aya wanasema, «Si uitunge na uizue wewe mwenyewe.» Waambie, ewe Mtume, Hili si langu, na haifai kwangu mimi nilifanye. Kwa kuwa Allah Mtukufu Ameniamuru kufuata wahyi nilioletewa kutoka Kwake. Nao ni hii Qur’ani ninayowasomea, inayokusanya hoja na dalili zinazotoka kwa Mola wenu na yenye ufafanuzi, inayoongoza Waumini kwenye njia iliyonyooka sawa, na ni rehema ambayo kwayo Allah Mtukufu Anawarehemu waja Wake Waumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net