Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 202

Al-A'raaf 7:202

الأعراف

وَإِخْوَٰنُهُمْ يَمُدُّونَهُمْ فِى ٱلْغَىِّ ثُمَّ لَا يُقْصِرُونَ

Maana

Na ndugu zao wanawavutia kwenye upotovu, kisha wao hawaachi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ndugu zao wanawavutia kwenye upotofu, kisha wao hawaachi. [202]

[202] Na ndugu zao mashetani, nao ni hao makafiri, mashetani huwazidisha upotovu kwa kuwajaza wasiwasi. Tena hawa makafiri hawaachi upotovu wao wakazingatia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ndugu wa mashetani, nao ni wapotofu miongoni mwa wapotevu wa wanadamu ambao mashetani wanawasukuma kwenye upotevu na upotofu. Na mashetani wa kijini hawaachi nafasi iwapite katika kuwasukuma kwao mashetani wa kibinadamu kwenye upotofu. Na mashetani wa kibinadamu hawaachi nafasi iwapite katika kuyafanya yale ambayo mashetani wa kijini wanayafanyia ushawishi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net