Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 204

Al-A'raaf 7:204

الأعراف

وَإِذَا قُرِئَ ٱلْقُرْءَانُ فَٱسْتَمِعُوا۟ لَهُۥ وَأَنصِتُوا۟ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

Maana

Na inaposomwa Qur-ani, basi isikilizeni na mnyamaze ili mrehemewe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na isomwapo Qur'ani isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa. [204]

[204] Enyi Waumini! Mkisomewa Qur'ani isikilizeni kwa masikio yenu, mpate kuzingatia mawaidha yake, na msikilize vizuri mpate kuipata rehema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na isomwapo Qur’ani isikilizeni, enyi watu, na mnyamaze ili muielewe kwa matarajio kwamba Allah Mtukufu Awarehamu kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net