Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 205

Al-A'raaf 7:205

الأعراف

وَٱذْكُر رَّبَّكَ فِى نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ ٱلْجَهْرِ مِنَ ٱلْقَوْلِ بِٱلْغُدُوِّ وَٱلْـَٔاصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ ٱلْغَـٰفِلِينَ

Maana

Na mkumbuke Mola wako Mlezi katika nafsi yako kwa unyenyekevu na hofu, na bila ya kuinua sauti juu kwa kauli, asubuhi na jioni, wala usiwe miongoni wa walioghafilika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkumbuke Mola Mlezi wako nafsini kwako kwa unyenyekevu na khofu, na bila ya kupiga kelele kwa kauli, asubuhi na jioni. Wala usiwe miongoni wa walio ghafilika. [205]

[205] Na mtaje Mola wako Mlezi ndani ya nafsi yako, upate kuhisi kuwa upo karibu na Mwenyezi Mungu, kwa kumnyenyekea na kumkhofu, bila ya kupiga makelele, bali juu kidogo kuliko kwa siri, na chini ya kudhihirisha kwa maneno. Na umtaje na umkumbuke asubuhi na jioni, ili uanzie mchana wako kwa kumkumbuka Mola wako Mlezi, na ukhitimishie kwayo vile vile. Na wakati wako wote usighafilike na kumtaja na kumkumbuka Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mtaje Mola wako, ewe Mtume, ndani ya nafsi yako kwa kumnyenyekea Allah Mtukufu na kumdhalilikia, hali ya kumcha Yeye moyoni, na umuombe kwa namna ya kati na kati baina ya kutoa sauti na kuifanya chini, katika mwanzo wa mchana na mwisho wake, na usiwe ni miongoni mwa wenye kughafilika kumtaja Allah Mtukufu na kupumbaa katika nyakati zao zinginezo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net