Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 206

Al-A'raaf 7:206

الأعراف

إِنَّ ٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِۦ وَيُسَبِّحُونَهُۥ وَلَهُۥ يَسْجُدُونَ ۩

Maana

Hakika wale walio kwa Mola wako Mlezi hawajivuni wakaacha kumuabudu, na wanamtakasa, na wanamsujudia Yeye.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walioko kwa Mola wako Mlezi hawajivuni wakaacha kumuabdu, na wanamtakasa na wanamsujudia [206]

[206] Hao walio karibu na Mola wako Mlezi kwa utukufu na takrimu hawatakabari wakaacha kumuabudu. Na wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kila lisio faa kwake. Na wanamnyenyekea Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walioko mbele ya Mola Wako miongoni mwa Malaika hawafanyi kiburi kwa kuacha kumuabudu Allah Mtukufu, bali wao wanafuata amri Zake, wanamtakasa mchana na usiku na wanamwepusha na mambo yasiyonasibiana na Yeye, na Yeye Peke Yake wanamsujudia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net