Al-A'raaf 7:149
الأعرافوَلَمَّا سُقِطَ فِىٓ أَيْدِيهِمْ وَرَأَوْا۟ أَنَّهُمْ قَدْ ضَلُّوا۟ قَالُوا۟ لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ
Na wakati mambo yalipoangushwa katika mikono yao, na wakaona ya kwamba wamekwishapotea, wakasema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hataturehemu na akatufutia dhambi, basi bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa waliohasiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walipo juta na wakaona ya kwamba wamekwisha potea, walisema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hakuturehemu na akatusamehe, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa walio khasiri. [149]
[149] Walipo tambua kuteleza kwao, na makaso yao, wakababaika, na wakajuta majuto makubwa kwa kumfanya ndama ndiye Mungu. Makosa yao yakabainika wazi, wakasema: Wallahi! Ikiwa Mola wetu Mlezi hakutusamehe hakika tutakuwa miongoni walio khasiri khasara iliyo dhaahiri; kwa vile kuabudu kisicho faa kuabudiwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walipojuta wale walioabudu ndama badala ya Allah Mtukufu pale aliporudi Mûsã kwao, na wakaona kwamba walipotea njia ya sawa, na waliondoka kwenye dini ya Allah Mtukufu, walianza kuukubali uja na kuomba kufutiwa makosa yao wakasema, «Mola wetu Asipoturehemu kwa kukubali toba yetu, na kufunika kwayo madhambi yetu, tutakuwa ni wenye kuangamia ambao matendo yao mema yamepita bure».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net