Al-A'raaf 7:148
الأعرافوَٱتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِنۢ بَعْدِهِۦ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُۥ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّهُۥ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا ۘ ٱتَّخَذُوهُ وَكَانُوا۟ ظَـٰلِمِينَ
Na kaumu ya Musa wakamfanya baada yake kutoka katika mapambo yao ndama mwenye kiwiliwili, mwenye kutoa mlio wa ng'ombe. Kwani hawakuona kuwa hawasemeshi wala hawaongoi njia yoyote? Walimchukua (kumuabudu), na wakawa madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na baada yake walimfanya ndama kutokana na mapambo yao (kumuabudu), kiwiliwili tu kilicho kuwa na sauti. Hivyo, hawakuona kuwa hawasemezi wala hawaongoi njia? Wakamuabudu, na wakawa wenye kudhulumu. [148]
[148] Na baada ya Musa kwenda kwenye mlima kusema na Mola Mlezi wake, kaumu yake walichukua vyombo vyao vya kujipamba wakatengeneza sura ya ndama, asiye na akili wala hatambui kitu. Lakini akitoa sauti mfano wa sauti ya ng'ombe, kwa namna walivyo muunda na ukipita upepo ndani yake. Na aliye waundia ni Saamiriyu (Msamaria). Naye akawaamrisha wamuabudu! Upumbavu gani huu wa akili zao! Hivyo wao walipo mfanya ndiye mungu wakamuabudu, hawakuona kuwa hawasemezi, wala hawezi kuwaongoa wafuate njia iliyo sawa? Hakika hawa wamejidhulumu nafsi zao kwa kitendo hichi kiovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walitengeneza watu wa Mûsã, baada ya yeye kuwaacha kwenda kuzungumza na Mola Wake, sanamu wa ndama asiye na roho anayetoa sauti, kutokana na dhahabu yao, wakamfanya ni muabudiwa. Kwani hawajui kwamba yeye hasemi na wao na hawaongozi wao kwenye kheri yoyote? Walijasiri kufanya jambo hili ovu, wakawa ni wenye kujidhulumu nafsi zao, ni wenye kuweka kitu mahala pasipokuwa pake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net