Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 136

Al-A'raaf 7:136

الأعراف

فَٱنتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَـٰهُمْ فِى ٱلْيَمِّ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا وَكَانُوا۟ عَنْهَا غَـٰفِلِينَ

Maana

Basi tukawaadhibu, tukawazamisha katika bahari kwa sababu walizikadhibisha Ishara zetu, na wakawa wanaghafilika mbali nazo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi tuliwapatiliza, tuka- wazamisha baharini kwa sababu walizikanusha Ishara zetu, na wakaghafilika nazo. [136]

[136] Tuliwateremshia nakama yetu. Tukawazamisha baharini kwa sababu ya kushikilia kwao kukanusha Ishara zetu, na hadi ya kutoyabali mafunzo ya Imani na ut'iifu yaliyomo katika hizo Ishara.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi tukawalipiza ulipokuja muda uliowekwa kwa wao kuangamizwa, kwa kuwashushia mateso yetu, nayo ni kuwazamisha baharini, kwa sababu ya kuikanusha kwao miujiza iliyodhihiri kwa Mûsã na wakawa wanaipuuza; na kupuuza huko ndio sababu ya kukanusha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net