Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 137

Al-A'raaf 7:137

الأعراف

وَأَوْرَثْنَا ٱلْقَوْمَ ٱلَّذِينَ كَانُوا۟ يُسْتَضْعَفُونَ مَشَـٰرِقَ ٱلْأَرْضِ وَمَغَـٰرِبَهَا ٱلَّتِى بَـٰرَكْنَا فِيهَا ۖ وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ ٱلْحُسْنَىٰ عَلَىٰ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ بِمَا صَبَرُوا۟ ۖ وَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُۥ وَمَا كَانُوا۟ يَعْرِشُونَ

Maana

Na tukawarithisha kaumu wale waliokuwa wakidhoofishwa, mashariki ya ardhi na magharibi yake ambayo tulibariki ndani yake. Na likatimia neno jema la Mola wako Mlezi juu ya Wana wa Israili, kwa vile walivyosubiri. Na tukayaangamiza yale aliyokuwa akiyafanya Firauni na kaumu yake, na yale waliyokuwa wakiyajenga.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukawarithisha watu walio kuwa wanadharauliwa mashariki na magharibi ya ardhi tuliyo ibariki. Na likatimia neno jema la Mola Mlezi wako juu ya Wana wa Israili, kwa vile walivyo subiri. Na tukayaangamiza aliyo kuwa akiyafanya Firauni na kaumu yake, na waliyo kuwa wakiyajenga. [137]

[137] Tukawapa watu ambao walikuwa wakidharauliwa katika Misri, nao ni Wana wa Israili, ardhi alio ipa baraka Mwenyezi Mungu kwa kuifanya ina rutba na kheri nyingi, tangu mashariki mpaka magharibi yake. Neno jema la Mwenyezi Mungu likatekelezwa kwa ukamilifu, na pia ahadi yake ya ushindi kwa Wana wa Israili, kwa sababu ya kuvumilia kwao dhiki. Na tukayateketeza majumba ya fakhari, na kila majenzi, na chanja za mimea ya kutambaa, na bustani, na pandio za mizabibu, waliyo kuwa wakisimamisha na kujenga akina Firauni na watu wake! Hiyo ndiyo shani ya Mwenyezi Mungu, na ametimiza kweli ahadi yake kwa Wana wa Israili.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Tukawarithisha wana wa Isrãîl, waliokuwa wakifanywa wanyonge, pande za mashariki na magharibi ya ardhi, nazo ni sehemu za miji ya Shãm, tulizozitia baraka kwa kutoa mazao na matunda na mito. Na limetimia neno jema la Mola wako, ewe Muhammad, kwa Wana wa Isrãîl kwa kuwapa utulivu katika ardhi kwa sababu ya kuvumilia kwao makero ya Fir‛awn na watu wake. Na tukayavunjavunja yale maamirisho na mashamba ambayo Fir‛awn na watu wake walikuwa wakiyatengeneza, na majengo na majumba na mengineyo waliokuwa wakiyajenga .

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net