Al-A'raaf 7:138
الأعرافوَجَـٰوَزْنَا بِبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱلْبَحْرَ فَأَتَوْا۟ عَلَىٰ قَوْمٍ يَعْكُفُونَ عَلَىٰٓ أَصْنَامٍ لَّهُمْ ۚ قَالُوا۟ يَـٰمُوسَى ٱجْعَل لَّنَآ إِلَـٰهًا كَمَا لَهُمْ ءَالِهَةٌ ۚ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ
Na tukawavusha bahari Wana wa Israili, kisha wakajia kaumu waliokuwa wanayaabudu masanamu yao. Wakasema, "Ewe Musa! Tufanyie mungu kama hawa walivyo na miungu." Musa akasema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojua kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukawavusha bahari Wana wa Israili, wakafika kwa watu wanao abudu masanamu yao. Wakasema: Ewe Musa! Hebu tufanyie na sisi miungu kama hawa walivyo kuwa na miungu. Musa akasema: Hakika nyinyi ni watu msio jua kitu [138]
[138] Wana wa Israili wakaivuka bahari kwa uangalizi wetu, na kuwaunga mkono na kuwafanyia mepesi mambo yao. Baada ya kwisha vuka waliwakuta kaumu wameshika ibada ya masanamu. Walipoona hivi yale waliyo kuwa wameyazoea kuwaona Wamisri wakiabudu masanamu yaliwaghilibu, wakamtaka Musa awafanyie nao masanamu wayaabudu, kama ilivyo kuwa wale kaumu wana masanamu yao wanayo yaabudu! Hapo hapo Musa a.s. aliwatahayarisha na kuwakanya, akasema: Hakika nyinyi ni watu wapumbavu, msio na akili! Hamjui ibada ya Haki, wala hamumjui Mungu anaye stahiki kuabudiwa!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwakatia Wana wa Isrãîl bahari, wakapita kwa watu waliokuwa wamekaa na kuendelea kuabudu masanamu wao. Wana wa Isrãîl wakasema, «Tufanyie, ewe Mûsã, sanamu tupate kumuabudu na kumfanya mungu kama hawa watu walivyo na masanamu wanaowaabudu.» Mûsã akawaambia, «Hakika yenu nyinyi,enyi watu, ni wajinga wa kujua utukufu wa Allah Mtukufu, na hamjui kwamba ibada haifai kufanyiwa yoyote isipokuwa Allah Mtukufu, Aliye Mmoja, Mwenye kutendesha nguvu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net