Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 139

Al-A'raaf 7:139

الأعراف

إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ مُتَبَّرٌ مَّا هُمْ فِيهِ وَبَـٰطِلٌ مَّا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Hakika hawa, haya waliyomo yatakujaangamia, na ni batili hayo waliyokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika haya waliyo nayo watu hawa yatakuja angamia, na hayo waliyo kuwa wakiyafanya yamepotea bure. [139]

[139] Hawa mnao waona wanaabudu masanamu, hapana shaka haya walio nayo ni yenye kuangamia, na hii dini waliyo nayo ni potovu , bure bilashi. Na a'mali zao ni zenye kupotea, wala hazibaki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika hawa wanaowakalia hawa masanamu, ushirikina waliomo ndani yake umeangamizwa, na ni yenye kuangamiza na ni ya urongo yale waliokuwa wakiyafanya ya kuwaabudu masanamu hao ambao hawawazuilii adhabu ya Allah Mtukufu ikiwashukia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net