Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 140

Al-A'raaf 7:140

الأعراف

قَالَ أَغَيْرَ ٱللَّهِ أَبْغِيكُمْ إِلَـٰهًا وَهُوَ فَضَّلَكُمْ عَلَى ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Akasema, "Je, niwatafutie mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye aliyewaboresha kuliko walimwengu wote?"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Je, nikutafutieni mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye aliye kufadhilisheni juu ya viumbe vyote? [140]

[140] Je, nikutafutieni wa kuabudiwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote, na Yeye ndiye aliye kupeni fadhila, na akakupeni neema asio pata kupewa mwengine asiye kuwa nyinyi katika zama zenu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsã akasema kuwaambia watu wake, «Je, niwatafutie muabudiwa asiyekuwa Allah Mtukufu, na Allah Mtukufu Ndiye Aliyewaumba na Akawatukuza juu ya walimwengu wa zama zenu kwa wingi wa Mitume watokanao na nyinyi, kumuangamiza adui yenu na kwa miujiza Aliyowahusu nayo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net