Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 141

Al-A'raaf 7:141

الأعراف

وَإِذْ أَنجَيْنَـٰكُم مِّنْ ءَالِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوٓءَ ٱلْعَذَابِ ۖ يُقَتِّلُونَ أَبْنَآءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَآءَكُمْ ۚ وَفِى ذَٰلِكُم بَلَآءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ

Maana

Na pale tulipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni waliowatia adhabu mbaya zaidi. Wakiwaua wavulana wenu, na wakiwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo yalikuwa majaribio makubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale tulipo kuokoeni kwa watu wa Firauni walio kupeni adhabu za mwisho wa uovu. Wakiwauwa wavulana wenu, na wakawaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo yalikuwa majaribio makubwa kutokana na Mola wenu Mlezi. [141]

[141] Kumbukeni alipo kuvueni Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa uangalizi wake na watu wa Firauni, walio kuwa wakikuadhibuni ukomo wa adhabu, wakikudhalilisheni muwatumikie katika kazi ngumu, wala hawakukuoneeni huruma kama wanyama, wakiuwa wavulana wenu na wakiwabakisha wasichana ili mzidi kudhoofika kwa wingi wa wanawake! Na katika adhabu za Firauni zilizo kushukieni, na kukuvueni nazo, pana mtihani mkubwa wa Mola wenu Mlezi, wala hapana mfano wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbukeni, enyi Wana wa Isrãîl, neema zetu kwenu tulipowaokoa na kifungo cha Fir‛awn na jamaa zake na unyonge na utwevu mliokuwa nao, wa kuchinjwa watoto wenu wa kiume na kuwaacha wanawake wenu ili watumike na wadharauliwe. Na katika kupitia kwenu mateso mabaya zaidi na maovu zaidi kisha kuwaokoa na mtihani utokao kwa Allah Mtukufu kwenu na neema kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net