Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 135

Al-A'raaf 7:135

الأعراف

فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ ٱلرِّجْزَ إِلَىٰٓ أَجَلٍ هُم بَـٰلِغُوهُ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ

Maana

Basi tulipowaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie, tazama! Wakavunja ahadi yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini tukiwaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie, mara wakivunja ahadi yao. [135]

[135] Tulipo waondolea adhabu kila mara kwa muda wao mpaka mwisho wake ukisha huivunja ahadi yao, na huenda kinyume na kiapo chao, na hurejea yale yale waliyo kuwa nayo. Kwao wao hayo majaribio ya kuwaachisha maovu hayakuleta faida!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Alipowaondolea adhabu Aliyoiteremsha kwao, mpaka muda ambao hapana budi wataufikia na waadhibiwe, ambapo hapo hakutawanufaisha kule kupewa muhula kuliotangulia na kuondolewa kwao adhabu mpaka wakati wa kufika kwake, punde si punde wanarudi kuvunja ahadi waliyomuahidi Mola wao na Mûsã na wanaendelea na kudumu na ukafiri wao na upotevu wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net