Al-A'raaf 7:12
الأعرافقَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسْجُدَ إِذْ أَمَرْتُكَ ۖ قَالَ أَنَا۠ خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِى مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُۥ مِن طِينٍ
(Mwenyezi Mungu) akasema, "Ni nini kilichokuzuia kusujudu nilipokuamrisha?" Akasema, "Mimi ni bora zaidi kumliko yeye. Uliniumba kwa moto, naye ulimuumba kwa udongo."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo [12]
[12] Mwenyezi Mungu kwa kuudhika naye kwa uasi wake alimwambia: Nini kilicho kuzuia usimtukuze Adam, na hali Mimi nimekuamrisha ufanye hivyo? Iblisi akajibu kwa inda na kiburi: Mimi bora kuliko Adam. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. Na moto ni mtukufu zaidi kuliko udongo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Akasema hali ya kumkemea Iblisi kwa kuacha kwake kumsujudia Ãdam, «Ni lipi lililokuzuia usisujudu nilipokuamuru?» Iblisi akasema, «Mimi ni bora kuliko yeye, kwa kuwa mimi nimeumbwa kwa moto na yeye ameumbwa kwa udongo.» Akaona kuwa moto ni bora kuliko udongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net