Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 11

Al-A'raaf 7:11

الأعراف

وَلَقَدْ خَلَقْنَـٰكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَـٰكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِـَٔادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ ٱلسَّـٰجِدِينَ

Maana

Na hakika tuliwaumba, kisha tukawatia sura, kisha tukawaambia Malaika, "Msujudieni Adam." Basi wakasujudu isipokuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa waliosujudu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu. [11]

[11] Na katika khabari za wale wa mwanzo pana mazingatio na mawaidha, yanayo dhihirisha kuwa Shetani anajaribu akuondoleeni neema kwa kusahau kwenu amri za Mwenyezi Mungu. Sisi tumemuumba baba yenu Adam, na tukampa sura. Kisha tukawaambia Malaika: Mtukuzeni! Wakamtukuza kwa kut'ii amri ya Mola wao Mlezi, ila Iblisi hakut'ii.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika, tumewaneemesha nyinyi kwa kumuumba chanzo chenu – naye ni baba yenu Ãdam- kutokana na kutokuwako kamwe, kisha tukamtia sura ya umbo lake lililo bora kuliko lile la viumbe wengi. Kisha tuliwaamuru Malaika wetu, (amani iwashukie,) wamsujudie kwa ajili ya kumtukuza na kumuheshimu na kuonyesha ubora wa Ãdam. Nao wakamsujudia wote, (isipokuwa Iblisi,) ambaye alikuwa pamoja na wao, hakuwa ni miongoni mwa wenye kumsujudia Ãdam kwa kumuhusudu kwa heshima hii kubwa aliyopewa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net