Al-A'raaf 7:10
الأعرافوَلَقَدْ مَكَّنَّـٰكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَـٰيِشَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ
Na hakika tumewaimarisha katika dunia, na tukawajalia humo njia za kupata maisha. Ni kidogo tu mnavyoshukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika tumekuwekeni katika ardhi, na tumekujaalieni humo njia za kupatia maisha. Ni kuchache kushukuru kwenu. [10]
[10] Nasi tumekuwekeni katika ardhi, na tukakupeni nguvu za kuiamirisha mkajipatia manufaa ndani yake, na tukakusahilishieni njia za kupatia maisha. Juu ya neema hizi zote, kumekuwa kuchache mno kumshukuru kwenu Mwenyezi Mungu. Nanyi mtakuja pata malipo ya hayo myatendayo!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika tumewapa utulivu, enyi watu, katika ardhi, na tumewaekea humo vitu mtakavyovitumia katika maisha yenu miongoni mwa vyakula na vinywaji; na pamoja na hayo, shukrani zenu juu ya neema za Mola wenu ni chache.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net